Idhaa ya Redio ya UM show

Idhaa ya Redio ya UM

Summary: no show description found

Join Now to Subscribe to this Podcast

Podcasts:

 Ban alaani shambulio nchini Libya | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amelaani vikali shambulio lililotokea katika hoteli iitwayo Corinthia mjini Tripoli mnamo Januari 27. Taarifa iliyotolewa na  msemaji wa Katibu Mkuu imesema Bwana Ban ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza wapendwa wao kufuatia shambulio hilo. Amesema ugaidi hauna nafasi katika Libya mpya na kwamba hautadhoofisha majadiliano [...]

 Mjumbe wa Umoja wa Mataifa alaani mashambulizi Gaza | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu utaratibu wa amani Mashariki ya Kati, Robert Serry, ameeleza kukasirishwa sana na mashambulizi dhidi ya ofisi yake, UNSCO, yaliyotokea asubuhi ya Jumatano hii huko Ukanda wa Gaza. Tukio hilo limefanyika wakati wa maandamano ambapo watu kadhaa wameruka ukuta wa ofisi hiyo na kuanza kuharibu majengo na mali za [...]

 Kamati ya haki za wabunge yaangazia bara la Asia | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mkutano wa siku nne wa kamati ya haki za binadamu kwa wabunge umefikia tamati huku ukipitisha  maamuzi muhimu yanayogusa maeneo mbali mbali duniani. Taarifa ya umoja wa mabunge duniani, IPU imetaja maamuzi hayo yamegusia mathalani Sri Lanka ambapo wajumbe wamesema ni matumaini yao kuwa serikali itachukua hatua muhimu kuwafiisha mbele ya sheria watuhumiwa wa mauaji [...]

 UNICEF na kampeni kuhusu haki za watoto | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

      Nchini Tanzania, serikali imejikuwa inajitahidi kuendeleza hali ya haki za watoto. Mafanikio hayo yamepongezwa katika mkutano wa 68 wa kamati ya haki za watoto unaoendelea mjini Geneva, Uswisi. Hata hivo, changamoto nyingi bado zipo, ikiwemo ndoa na mimba za utotoni. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na Mtandao wa Wanahabari [...]

 UM Tanzania na kumbukizi ya mauaji ya Holocaust | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Kumbukizi ya miaka 70 ya kukombolewa kwa Auschwitz Birkenau zimefanyika maeneo mbali mbali duniani ikiwemo Tanzania ambapo Stella Vuzo Afisa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa ameieleza Idhaa hii kile walichofanya leo jijini Dar es salaam. (Sauti ya Stella) Na kwa mantiki hiyo lengo ni kuhakikisha.. (Sauti ya Stella)

 Safari ya kujenga kustahimiliana bado ni ndefu: Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ghasia na upendeleo unaodhihirika kila siku vinakumbusha dunia kuwa safari ya kusimamia haki, kuepusha mauaji ya kimbari na kutetea utu wa binadamu bado ni ndefu. Ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliotoa leo ikiwa ni miaka 70 tangu majeshi ya washirika yakomboea kambi ya mateso ya Auschwitz Birkenau, ambayo utawala [...]

 Waasi Sudan Kusini waanza kuachilia huru watoto wanaowatumikisha: UNICEF | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau wake wamefanikisha mpango wa kuachiliwa huru kwa watoto wapatao 3,000 wanaotumikishwa na vikundi vilivyojihami nchini Sudan Kusini, ikieleza kuwa hiyo ni idadi kubwa zaidi kuwahi kufikia hatua hiyo. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) UNICEF inasema tayari kundi la kwanza la watoto [...]

 Ukata kusitisha ujenzi wa makazi ya wapalestina :UNRWA | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestine, UNRWA, limelazimika kusitisha mpango wake wa msaada wa kifedha huko Gaza kwa mamia ya maelfu ya watu kwa ajili ya kukarabati nyumba zao zilizoharibiwa pamoja na ruzuku ya kodi kwa wasio na makazi. Abdullahi Boru na ripoti kamili. (Taarifa ya Abdullahi) Zaidi ya nyumba 96,000 za familia  [...]

 Zeid alaani mauaji ya watu 20 Misri | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

  Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein ameelezea kusikitishwa kwake na vifo vya watu 20 wakati wa mapambano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama nchini Misri ijumaa. Akiongea mjini Geneva Kamishna Zeid ameitaka mamlaka za Misri kuchukua hatua za dharura kukomesha matumizi ya nguvu za ziada [...]

 UNMISS yalaani shambulio lililouwa watu 11 wakiwamo wanahabari | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

  Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umelaani vikali mauaji ya raia kumi na mmoja,  watano miongoni mwa wakiwa ni wanahabari ambao walishambuliwa barabarani wakati wakiwa wanasafiri kuelekea Raja jimboni Bahr El Ghazal Magharibi  Kwa mujibu wa taarifa ya UNMISS watu wasiofahamika na amboa walijihami kwa silaha walifyatua risasi katika msafara huo [...]

 Watoto Ukraine walazimika kuishi makazi ya kuzuia bomu- UNICEF | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

  Mapigano yanayoendelea nchini Ukraine yamewalazimu watoto wapatao 1,000 na familia zao kuhamia kwenye makazi ya kuwalinda kutokana na mabomu kwenye mji wa Donetsk, mashariki mwa nchi, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. UNICEF imesema kuna hatari kubwa kiafya ya kuzuka magonjwa kama vile ule wa kupooza, yaani polio, kwa watoto [...]

 Huduma za afya kadhia Uganda | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Huduma za afya zimekuwa changamoto kubwa hususani kwa nchi zinazoendelea ambapo wanaothirika zaidi ni wanawake hasa wajawazito wakati wanapojifungua. Nchini Uganda hali ikoje? Ungana na John Kibego kufahamu kadhia wanazokutana nazo wananchi wa maeneo hayo.  

 Balozi Kamau azungumzia uamuzi wa ICC kuhusu Kenyatta | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Siku ya Ijumaa tarehe Tano Disemba mwaka 2014, mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC huko The Hague, Uholanzi ilitupilia mbali mashtaka dhidi ya Uhuru Kenyatta. Mwendesha Mashtaka Mkuu Fatou Bensouda alieleza kuwa uamuzi huo unazingatia kuwa hawana ushahidi wa kutosha wa kuweza kuthibisha pasipo shaka mashtaka matano yaliyokuwa yanamkabili Kenyatta. Kufuatia uamuzi huo, Joseph Msami [...]

 Vichochezi na harakati dhidi ya maambukizi ya ukimwi | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ukimwi ugonjwa ulioanza kutikisa dunia miaka ya 1980 na kusababisha vifo vya maelfu ya watu, sasa angalau kuna nuru kutokana na matibabu dhidi ya magonjwa nyemelezi na hata huduma za upimaji ili watu waweze kufahamu afya zao. Kutokana na umuhimu wa harakati za kutokomeza ugonjwa huo, Umoja wa Mataifa uliamua kuwa kila tarehe Mosi ya [...]

 Tujitolee kwa maendeleo yetu na ya nchi :Vijana | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Tarehe 5 Mwezi Disemba kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kujitolea siku ambayo hutumiwa na jumuiya ya kimataifa kuhamasisha kujitolea kwa maendeleo ya jamii. Kauli mbiu ya madhimisho ya mwaka huu ni sababisha mabadiliko jitolee.Wakati siku hii ikiadhimishwa utamaduni bado ni jambo geni katika nchi zinazoendelea. Joseph Msami amefanya mahojiano na baadhi ya watu [...]

Comments

Login or signup comment.