Idhaa ya Redio ya UM show

Idhaa ya Redio ya UM

Summary: no show description found

Join Now to Subscribe to this Podcast

Podcasts:

 Maelfu ya raia wa DRC wakimbia Katanga, UNHCR yaingiwa hofu | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeeleza wasiwasi wake juu ya ghasia zinazosababisha hali mbaya ya kibinadamu kwenye jimbo la Katanga nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Taarifa  kamili na Amina Hassan (Taarifa ya Amina)  UNHCR imesema ghasia zilizotokea katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita zimesababisha wakimbizi wapya 71,000 ambao ni kando [...]

 Msafara wa Umoja wa Mataifa washambuliwa Iraq | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Msafara wa magari ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI, umeshambuliwa karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa Baghdad. Nibu  msemaji wa Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Farhan Haq amewaambia waaandishi wa habari mjini New York kuwa hakuna aliyeuwawa au kujeruhiwa katika shambulio hilo licha ya kuwa moja kati ya ya magari [...]

 Kutesa aisifu kazi ya Baraza la Haki za Binadamu | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limesikiliza ripoti ya kila mwaka ya Baraza la Haki za Binadamu, ambayo imewasilishwa na Rais wa Baraza la Haki za Binadamu, Baudelaire Ndong Ella. Akizungumza kabla kumkaribisha Bwana Ndong Ella kutoa ripoti hiyo, Rais wa Baraza Kuu, Sam Kutesa, amesisitiza umuhimu wa Baraza la Haki za Binadamu "Kwa [...]

 Wakosoaji nusura walinishawishi kukata tamaa- mshindi wa tuzo ya Sayari Dunia | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mwanaharakati wa mazingira ambaye ameshinda tuzo ya Umoja wa Mataifa ya 'Bingwa wa Sayari Dunia' kufuatia mpango wake wa kusafisha bahari amesema mara kwa mara alitaka kukata tamaa kwa sababu alikumbana na kukosolewa mno. Boyan Slat, ambaye alisitisha masomo yake ya chuo kikuu kwa muda ili akabiliane na tatizo la kuondoa taka za plastiki baharini, [...]

 Ban aitaka serikali ya Sudan kuruhusu UNAMID kulizuru eneo la Thabit | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea masikitiko yake kuhusiana na madai ya ubakaji wa halaiki katika eneo la Thabit, Darfur Kaskazini. Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID  ulitembelea Thabit tarehe 9 Novemba, lakini uwepo mzito wa kijeshi na polisi ulifanya uchunguzi wa kina kuwa [...]

 Ronaldo, Neymar, Drogba na Lahm washiriki juhudi za kuongeza uelwa kuhusu Ebola | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Wachezaji bora wa Kandanda, ikiwa ni pamoja na nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, Neymar Jr. kutoka Barcelona, Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba na Philip Lahm wa Bayern Munich, wamejiunga na vikosi vya pamoja na wataalam wa afya wa kimataifa ili kusaidia kuongeza uelewa wa kimataifa katika mapambano dhidi ya Ebola. Katika taarifa kwa vyombo [...]

 UNMEER yaomboleza Kifo cha Rudasingwa | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kushughulikia Dharura ya Ebola, UNMEER, unaomboleza kifo cha Marcel Rudasingwa- Naibu Katibu Mkuu ambaye pia alikuwa Meneja wa dharura wa Ujumbe huo nchini Guinea. Katibu Mkuu alimteua Rudasingwa, raia wa Rwanda, tarehe 8 Oktoba kuchukua nafasi hiyo, lakini aliaga dunia ghafla kutokana na sababu za kiasili hii leo. Katika [...]

 Fahamu kuhusu kisukari | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ugonjwa wa kisukari ni miongni mwa maugonjwa yasiyo ya uambikzwa na husababishwa na mambo mbali mbali ikiwemo mienendo ya maisha. Kufahamu zaidi juu ya ugonjwa huu ikiwamo namna ya kukabiliana nao na undani wa visababishi vyake, ungana na Geoffrey Onditi wa Radio washirika KBC nchini Kenya katika mahojiano maalum.

 UNICEF wawezesha ustawi wa watoto Kenya | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau mbalimbali mathalani serikali zinahakikisha ustawi wa watoto katika hatua mbalimbali za ukuaji wao. Nchini Kenya shirika hilo linatoa usaidizi kwa watoto katika kuhakikisha wanapatiwa huduma bora ili kuwezesha ukuaji wao na kujenga jamii bora. Ungana na Amina Hassan katika makala  ifuatayo.

 Machafuko Iraq yasababisha madhila kwa raia: OCHA | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Machafuko yanayoendelea nchini Iraq yamesabaabisha zaidi ya watu milioni moja na laki tisa kupoteza na kuhamia katika sehemu tofauti . Taarifa zaidi na Joseph Msami (TAARIFA YA MSAMI) Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaaada ya kibinadamu OCHA, mapigano yanayoendelea hususani vuguvugu la kundi la dola ya kiisilamu  ISIL limesabisha mtawanyiko [...]

 Watu 370,000 hufariki dunia kila mwaka kwa maji –WHO | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni WHO imesema kuwa kwa wastani zaidi ya watu 370,000 hufariki dunia kila mwaka kwa maji wanapozama, huku ikitaja pia hatari inayowaandama watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Taarifa kamili na Joshua Mmali (Taarifa ya Joshua) Ripoti hiyo imebainisha maeneo ambayo matukio hayo yanajitokeza ni pamoja [...]

 Hali ya sasa kuhusu mzozo wa Ukraine si endelevu -Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuwa ulimwengu umegawanyika kuhusu mzozo wa Ukraine kama nyakati za vita baridi, na kuonya kuwa hali hiyo ya sasa haiwezi kuwa endelevu kwa ajili ya amani ya dunia nzima na uchumi. Katibu Mkuu amesema hayo wakati mkutano wa siku mbili wa nchi 20 tajiri zaidi duniani [...]

 Tahadhari: Ebola yatishia kudidimiza maendeleo- ripoti ya UM | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Umoja wa Mataifa umoenya kuwa taifa la Sierra Leone linapaswa kujiandaa kwa madhara ya kijamii na kiuchumi yatokanayo na tatizo la homa ya Ebola, kufuatia ripoti mpya ya utafiti uliofadhiliwa na Shirika la Mpango wa Maendeleo katika Umoja wa Mataifa, UNDP, Wizara ya Fedha na Maendeleo ya Kiuchumi Sierra Leone, Benki ya Dunia, Benki ya [...]

 Ban awapa heko raia wa Burkina Faso kuafikia katiba ya mpito | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katiba Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewapa heko watu wa Burkina Faso kufuatia kuafikia kwa pamoja katiba ya mpito, ambayo itatoa mwongozo wa kisheria kwa serikali ya kiraia ya mpito, hadi wakati wa uchaguzi mnamo Novemba mwaka 2015. Bwana Ban amesema anatazamia kuona kusainiwa kwa katiba hiyo, kuteuliwa na kusimikwa kwa rais wa [...]

 Vijana Tanzania kunufaika na siku ya idaid ya watu:UNFPA | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Tarehe 18 Novemba kila mwaka ni siku ya kimataifa ya idadi ya watu. Siku hii hutumiwa kufahamu idadi ya watu duniani na  huku takwimu hizo zikitumiwa kupanga  mikakati ya ustawi wa watu  duniani kote. Maudhui ya siku hiyo mwaka huu ni ustawi wa vijana kundi ambalo ni nguvu kazi katika jamii. Shirika la idadi ya [...]

Comments

Login or signup comment.