Idhaa ya Redio ya UM show

Idhaa ya Redio ya UM

Summary: no show description found

Join Now to Subscribe to this Podcast

Podcasts:

 Ebola bado ni janga tuongeze usaidizi; Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amehutubia mkutano wa viongozi wa nchi za Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN huko Myanmar akiomba nchi hizo kuimarisha jitihada zao za kukabiliana na mlipuko wa Ebola huko Afrika Magharibi. Taarifa kamili na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Ban pamoja na kushukuru usaidizi wa baadhi ya nchi kwenye [...]

 Wakati UNMEER ikifikiria kubadili mwelekeo wa huduma, daktari huko Mali aambukizwa Ebola | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia dharura ya Ebola, UNMEER, Anthony Banbury amesema kadri mlipuko wa Ebola unavyobadili mwelekeo ni vyema kwenda na wakati na kutoa huduma kuligana na mazingira. Amesema hayo wakati huu ambapo idadi ya watu waliofariki dunia kutoka na Ebola imefikia 5,160 kati ya wagonjwa zaidi ya Elfu Kumi [...]

 Athari za mabadiliko ya Tabianchi ni wazi, ni lazima tuchukue hatua za haraka: Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ripoti ya tano ya Jopo la Kimataifa kuhusu Tabianchi , IPCC iliyotolewa Jumapili huko Copenhagen, Denmark imesema shughuli za binadamu zinazoathiri tabianchi zinazidi kuongezeka na athari zake kwa tabianchi ziko bayana kila bara. Imetaka hatua za haraka zichukuliwe ikiwemo uamuzi mgumu wa kisiasa ili kuwepo na hatma endelevu. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo [...]

 Baraza la Usalama lalaani vitendo vya ISIL Iraq | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani utekaji nyara na mauwaji ya  jamii ya Wasunni yaliyotekelezwa na wanamgambo wanaotaka kuweka dola la Uislamu wenye msimamo mkali, ISIL katika mkoa wa Anbar nchini Iraq. Miili ya waliouawa ilipatikana katika makaburi ya halaiki. Wengi wa wale waliouawa wamekuwa wakipambana na ugaidi kwa kushirikiana na [...]

 Vita, mizozo na majanga vyatishia MDGs Afrika:Ripoti | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ripoti mpya iliyozinduliwa  Jumamosi kwenye warsha ya kiuchumi barani Afrika huko Addis Ababa Ethiopia imesema wakati idadi ya Waafrika wanaofurahia viwango vya juu maishani ikiongezeka, nchi za Afrika zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara ni lazima ziongeza juhudi zao za kuhakikisha mizozo ya kisiasa, majanga na magonjwa kama vile Ebola huko Afrika Magharibi haziathiri mafanikio [...]

Comments

Login or signup comment.