Idhaa ya Redio ya UM show

Idhaa ya Redio ya UM

Summary: no show description found

Join Now to Subscribe to this Podcast

Podcasts:

 Ebola bado ni tishio kubwa: Nabarro | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ugonjwa wa Ebola bado ni tishio kubwa, wameonya watalaam wa Umoja wa Mataifa wakisema mazishi yasiyozingatia kanuni za afya yamesababisha ongezeko la idadi ya maambukizi mapya. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola, David Nabarro, amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana, maambukizi mapya yanaendelea kwa sababu watu [...]

 UNICEF yahaha kuwanususru wahanga wa mafuriko Malawi | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Baada ya kuwa na wakati mgumu kufuatia  mafuriko, wakazi wa Malawi sasa wanapatiwa misaada ya kibinadamu ikiwamo vyombo vy a ndani na malazi. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau kadhaa wanahakikisha maisha ya watu hawa yanarejea kuwa ya kawaida. Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo.

 Baraza lalaani vikali mashambulizi ya Boko Haram | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mwendelezo wa mashambulio yanayofanywa na kikundi cha kigaidi cha Boko Haram dhidi ya raia na askari. Miongoni mwa mashambulio hayo niyale ya tarehe Tatu na Nne Februari kwenye mpaka kati ya Nigeria na Cameroon ambako askari wa 26 na raia waliuawa na wengine walijeruhiwa. [...]

 Ufuatiliaji wa kuenea kwa Ebola bado changamoto:Ging | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mkurugenzi wa operesheni za ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na usaidizi wa kibinadamu, OCHA, John Ging amesema kuongezeka kwa visa vipya vya Ebola siku za karibuni huko Liberia, Guinea na Sierra Leone kumeibua hoja kuhusu uthabiti wa hatua za kufuatilia watu wote waliokuwa na makaribiano na wagonjwa wa Ebola. Akizungumza na waandishi wa habari [...]

 Uteuzi: Mladenov kumrithi Serry Mashariki ya Kati | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Nikolai Mladenov wa Bulgaria kuwa mratibu maalum wa mchakato wa amani Mashariki ya Kati. Mladenov anachukua nafasi ya Robert Serry ambaye Bwana Ban amemshukuru kwa mchango wake akishika wadhifa huo. Kwa sasa Mladenov ni mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu huko Iraq na mkuu wa ujumbe wa [...]

 Mtaalam wa UM aitaka Ulaya iruhusu wahamiaji kuingia kwa njia halali | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Muungano wa mataifa ya Ulaya, EU, ni lazima uwekeze katika uhamiaji ili wahamiaji waweze kuingia kwa njia halali na urejeshe udhibiti wa mipaka yake, amesema Mtaalam Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wahamiaji, François Crépeau, mwishoni mwa ziara yake rasmi kwa makao makuu ya EU, mjini Brussels, Ubeljiji. Crépeau amesema, kwa kuendelea kuwekeza [...]

 Maendeleo yoyote ya jamii yajali utu wa binadamu: Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika tukio maalum la maadhimisho ya miaka 20 tangu mkutano wa dunia kuhusu maendeleo ya jamii huko Copenhagen, Denmark ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema umaskini bado ni jambo ambapo kizazi cha sasa kinapaswa kutokomezwa. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Hotuba [...]

 Licha ya matumaini, hali ya Guinea Bissau haijatulia | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Nchini Guinea Bissau, kuna matumaini ya kurejesha utulivu na maridhiano nchini humo, serikali ikijitahidi kuimarisha mamlaka za kitaifa, kwa mujibu wa ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyojadiliwa leo katika Baraza la Usalama. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini Guinea Bissau, Miguel Trovoada, ambaye pia [...]

 Msadidizi wa rais Yemen aachiliwa huru | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen, James Benomar, amekaribisha taarifa ya kuachiliwa huru kwa msaidizi wa rais nchini Yemen, siku ya jumatano. Ahmed Bin Mubarak, mkurugenzi wa ofisi ya rais wa Yemen alikuwa ametekwa nyara kwa kipindi cha siku 10 na kundi la upinzani la Ansarallah. Benomar ameeleza kwamba kuachiliwa huru kwa kiongozi [...]

 Mpango wa EU kuibua ajira Milioni 2.1 Ulaya: ILO | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Kazi Duniani, ILO limesema zaidi ya fursa za ajira mpya Milioni 2.1 mpya zitapatikana kufikia katikati ya mwaka wa 2018 kutokana na mpango wa miaka mitatu wa uwekezaji uliowasilishwa na Rais wa Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker. Ripoti ya ILO iitwayo Mkakati wa uwekezaji uliojikita katika kutengeneza nafasi za ajira, inaonyesha kuwa uwekezaji [...]

 Miaka 70 baada ya Auschwitz Birkenau bado tunachukiana:Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumatano limekuwa na tukio maalum la kumbukizi ya wahanga wa mauaji ya Holocaust yaliyofanywa na manazi wa kijerumani miaka 70 iliyopita ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amesema kiwango kile cha mauaji kinatisha hadi leo hii. Kambi ya Auschwitz Birkenau ambayo ilikuwa kitovu cha mauji hayo ilikombolewa na majeshi ya [...]

 Twapongeza hatua ya Uholanzi kuhusu wahamiaji: Wataalamu | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu wamepongeza uamuzi wa serikali ya Uholanzi wa kupatia fedha manispaa nchini humo ambazo zinapatia maeneo ya kuishi wahamiaji wasio na makazi.Uamuzi huo unawapatia haki ya maisha yenye utu wahamiaji walioko nchini humo kihalali au kinyume cha sheria, haki inayojumuisha pia chakula, mavazi na malazi. Katika taarifa [...]

 MINUSMA yachunguza vifo vilivyotokea Gao | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA, unaanza kuchunguza vifo vilivyotokea wakati wa maandamano yaliyofanyika jumanne, mjini Gao. Stephane Dujarric, msemaji wa Umoja wa Mataifa, amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York. Amenukuu MINUSMA ikieleza kuwa ilitumia mabomu ya kutoa machozi na kufyatua risasi hewani ili kuzuia waandamanaji wasiingie kwenye jengo [...]

 Umoja wa Mataifa walaani vurugu kusini mwa Lebanon | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Jumatano asubuhi, maroketi yalirushwa nchini Israel kutoka upande wa Lebanon, jeshi la Israel likijibu kwa kufyatua risasi, amesema Stephen Dujaric msemaji wa Umoja wa Mataifa alipoongea na waandishi wa habari siku ya Jumatano. Amesema mlinda amani mmoja wa Umoja wa Mataifa ameuawa wakati wa mashambulio hayo na kwamba uchunguzi unaendelea ili kufahamu sababu ya kifo [...]

 Elimu ya chekechea yapigiwa chepuo Msumbiji | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Benki ya dunia kwa kushirikiana na washirika wa elimu wanapigia chepuo elimu ya awali, maarufu kwa jina chekechea nchini Msumbiji. Lengo ni kuhakikisha watoto wengi kadri iwezekanavyo wanajiunga na chekechea kabla ya kuijunga na elimu ya msingi nchini humo. Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayao.

Comments

Login or signup comment.