Idhaa ya Redio ya UM show

Idhaa ya Redio ya UM

Summary: no show description found

Join Now to Subscribe to this Podcast

Podcasts:

 COP20 iweke mustakhbali sawia wa mazingira: Muyungi | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Wakati mkutano wa 20 wa nchi wanachama kuhusu masuala ya mazingira, COP20 unaendelea huko Lima, Peru wawakilishi wa nchi mbali mbali wamekutana kushiriki katika majadiliano ya kuwezesha kufikiwa kwa mkataba wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi baadaye mwakani huko Paris, Ufaransa. Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira kwenye ofisi ya Makamu [...]

 Kinachoendelea Misri chatutia hofu:OHCHR | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ofisi ya  haki za  binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imesema ina wasiwasi mkubwa na mambo yanayojitokeza nchini Misri na athari zake kwenye uhuru wa kujieleza na kukusanyika. Wasiwasi huo unafuatia matukio ya mwishoni mwa wiki ambapo ambapo takribani watu watano wakiwemo maafisa usalama wawili waliuawa wakati wa mapigano kati ya waandamanaji na vikosi vya [...]

 Aina mpya za utumwa ni janga kwa mamilioni duniani:ILO | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ikiwa leo ni siku ya kumbukizi ya kumalizika kwa biashara ya utumwa ya kupitia bahari ya Atlantiki, Shirika la kazi duniani, ILO limetaka kasi zaidi iongezwe kuhakikisha aina mpya za utumwa ikiwemo utumikishaji kwenye ajira vinatokomezwa ifikapo mwishoni mwa karne hii.ILO imesema licha ya mafanikio kwenye harakati za kuondokana na vitendo hivyo, bado kazi ni [...]

 FAO yapokea msaada wa kukuza kilimo | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limepokea msaada wa zaidi ya Euro milioni tano kutoka serikali ay Ubelgiji  kwa ajili ya kusaida shughuli za shirika hilo za kulinda kilimo  cha kuinua kipato kwa ajili ya usalama wa chakula na uwezo wa kukabiliana na majanga asilia na migogoro ya kibinadamu.Taarifa kamili na [...]

 Ebola yabinya ukuaji wa uchumi: Ripoti | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mlipuko wa Ebola unaendelea kukwamisha ukuaji wa uchumi kwa nchi zilizokumbwa na ugonjwa huo, imesema ripoti mpya ya Benki ya dunia ikisema hali ni mbaya zaidi Guinea, Liberia, na Sierra Leone. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Ripoti hiyo imetolewa leo wakati Rais wa Benki ya dunia Jim Yong Kim akianza ziara yake [...]

 Tukomeshe aina zote za utumwa: Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

  Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga wa utumwa na biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki kauli mbiu ikiwa ni ushindi dhidi ya utumwa kuanzia Haiti na kwingineko, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitolea wito serikali, asasi za kiraia na sekta binafsi kuungana kukomesha aina zote za [...]

 Tutafanya kila tuwezalo kukomesha Ebola- Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewaambia waandishi wa habari mjini Washington, D.C kuwa, Umoja wa Mataifa utafanya kila uwezalo kuzisaidia nchi zilizoathiriwa na Ebola kuukomesha mlipuko wa homa hiyo, kuwatibu walioambukizwa, kuhakikisha kuwa huduma zote muhimu zinatolewa, na kutunza ustawi wa nchi na kuzuia kuenea kwa kirusi hicho katika nchi zingine. Ban [...]

 Ebola na taswira mkanganyiko, UNMEER sasa yajielekeza Mali | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Taswira ya mwelekeo wa mlipuko wa Ebola ni mchanganyiko wa matumaini na hofu, amesema mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola, David Nabarro wakati akihutubia Baraza la usalama la Umoja huo lililokutana kujadili amani na usalama barani Afrika , angazio likiwa ni Ebola. Amewaambia wajumbe kuwa ushiriki wa jamii kwenye vita dhidi ya Ebola [...]

 ICN2 yatamaishwa, Sierra Leone yazungumzia mahitaji muhimu dhidi ya Ebola | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mkutano wa pili wa kimataifa wa lishe umefunga pazia huko Roma, Italia ambapo mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani, FAO Jose Graziano da Silva amesema mkutano huo umefungua njia kwa nchi kukubaliana ajenda za kutokomeza njaa na utapiamlo. Bwana da Silva amesema anaamini muongo ujao unatakiwa utambuliwe kama muongo wa maendeleo, na [...]

 Fikra potofu dhidi ya matumizi ya choo zitokomezwe:UM | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Tarehe 19 mwezi Novemba kila mwaka ni siku ya vyoo duniani. Siku hii imetengwa kwa ajili ya kuchukua hatua na kuhamasisha uelewa kuhusu watu ambao hawana vyoo, hii ikiwa ni haki ya kila mwanadamu. Mwaka huu, kauli mbiu ya siku hii iliyotambuliwa rasmi na Baraza Kuu mwaka 2013, ni usawa na hadhi. Kampeni inalenga kuchagiza [...]

 #IMAGINE yapata chepuo, kibao Chiquitita kunufaisha wasichana | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Tarehe 20 Novemba katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kulifanyika tukio maalum lililosheheni tumbuizo kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 25 ya mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto. Watoto, watu wazima, wanadiplomasia walishiriki katika tukio hilo lililojumuisha uzinduzi wa mradi wa #IMAGINE wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, mradi [...]

 FAO yazindua tovuti mpya ya miongozo kuhusu mlo | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Kilimo na Chakula, FAO limezindua tovuti mpya ya miongozo kuhusu mlo, ambayo itakuwa kama jukwaa la kubadilishana taarifa kuhusu mienendo bora ya lishe kote duniani. Tayari, tovuti hiyo imeanza kukusanya miongozo ya lishe kutoka zaidi ya nchi 100, na itaendelea kuongezewa maelezo pale miongozo mipya inapoandaliwa na kusahihishwa. Miongozo kuhusu mlo katika chakula [...]

 Mwezi wa Oktoba 2014 ulivunja rekodi ya joto- WMO | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Viwango wastani vya joto duniani mwezi Oktoba mwaka huu, vilikuwa juu zaidi na kuweka rekodi mpya tangu nyaraka za viwango vya joto duniani zilipoanza kuwekwa mnamo mwaka 1880, limesema shirika la masuala ya hali ya hewa, WMO. WMO imesema, viwango vya joto baharini na nchi kavu vilikuwa juu zaidi kwa wastani, vikichukuliwa kwa ujumla kwa [...]

 Leo ni siku ya televisheni duniani, UNESCO yasisitiza umuhimu wake | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Leo ni siku ya televisheni duniani ikiangazia umuhimu wa chombo hicho cha mawasiliano katika kufikisha ujumbe kwa jamii. Umoja wa Mataifa unasisistiza siyo kifaa chenyewe bali filosofia inayotolewa na chombo hicho kinachowakilisha alama ya mawasiliano na utandawazi katika ulimwengu wa sasa. Katibu mtendaji wa tume ya taifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu [...]

 Mzozo Yerusalem Magharibi, Ban azungumza na viongozi wa Israel na Palestina | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo kwa njia ya simu kwa nyakati tofauti na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, na Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas kufuatia shambulio la hivi karibuni huko Yerusalem Magharibi. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema katika mazungumzo hayo Ban ameeleza kushtushwa kwake na [...]

Comments

Login or signup comment.