Idhaa ya Redio ya UM show

Idhaa ya Redio ya UM

Summary: no show description found

Join Now to Subscribe to this Podcast

Podcasts:

 Watu wenye msimamo mkali wanatumia dini kinyume na mafunzo: Al-Nasser | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu jumuiko la ustaarabu, Nassir Abdulaziz Al-Nasser amesema nchini Iraq na Syria dini na tamaduni tofauti zinakabiliwa na mashambulizi yaliyojizatiti. Akimwakilisha Katibu Mkuu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mkutano wa Muungano dhidi ya Unyanyasaji nchini Iraq na Syria uliofanyika huko Vienna, Austria, Bw Al-Nasser amesema [...]

 Kuna sababu lukuki za kupigia chapuo siku ya choo duniani: Eliasson | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Kuna sababu za kiuchumi, na kijamii kujadili umuhimu wa usafi na maji katika kuadhimisha siku ya choo duniani amesema naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson. Akiongea na waandishi wa habari mjini New York Bwana Eliasson amesema ikiwa maji na usafi utazingatiwa huongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa jamii husika. Naibu Katibu Mkuu [...]

 Kongamano kuhusu lishe laanza Roma | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Kongamano lililoandaliwa na Shirika la Chakula Duniani FAO limeanza leo huku likitilia uzito juu ya uwepo wa lishe bora kwa maelezo kuwa ndiyo ufunguo sahihi wa maisha bora. Kongamano hilo ambalo ni la pili linalofanyika katika makao makuu ya FAO Roma na linawaleta pamoja wajumbe kutoka sehemu mbalimbali duniani watakaojadiliana kuhusu umuhimu wa lishe kwa [...]

 UN yatilia shaka kuachiliwa haraka mtu alihusika na mauaji ya Bosnia | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake baada ya mtu aliyepatikana na hatia ya kushiriki mauaji ya halaiki katika ukanda wa Balkan kuachiliwa huru katika kipindi kifupi tangu alipotiwa hatiani. Mila Trbic alihukumiwa kwenda jela miaka 30 mnamo mwaka 2009 baada ya mahakama kuu ya serikali ya Bosnia kumtia hatiani kutokana na kushiriki mauji hayo.Maelfu ya [...]

 Serikali nyingi duniani zimeanza kupiga hatua –ILO | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani ILO Emmanuel Julien amesifu namna maneneo mbalimbali duniani yalivyopiga hatua kuwa kuweka sera na kutekeleza mikakati ambayo imefanikisha masuala ya kazi na uzalishaji wa ajira. Julien ambaye anahusika zaidi na kitendo cha ujasilimali ndani ya ILO amesema kuwa kumeendelea kushuhudiwa mabadiliko makubwa ya kutia moyo ikiwamo kwa serikali [...]

 IAEA yakamilisha ziara ya ukaguzi Zimbabwe | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Maofisa waandamizi ambao ni wataalamu masuala ya nyuklia na uzuiaji wa mionzi leo wamekamilisha ziara ya siku kumi nchini Zimbabwe iliyokuwa na lengo la kukagua namna nchi hiyo inavyozingatia mwongozo uliotolewa na Shirika la Nguvu la Atomiki la Umoja wa Mataifa IAEA kwa nchi kuzingatia usalama wa mionzi na masuala mengine. Taarifa kamili na George [...]

 Umoja wa Mataifa walaani shambulio katika sinagogi Jerusalem | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani mashariki ya kati Robert Serry ameeleza kuchukizwa na shamblio la asubuhi ya leo katika hekalu mashariki mwa Jerusalem. Mratibu huyo maalum amesisitiza katika taarifa yake kuwa Umoja wa Mataifa unatoa wito wa dharura kwa pande zote kufanya kila liwezekanalo kuepusha kuendelea kwa hali liyopo ya [...]

 UNESCO yawataka wanaozozana Libya kulinda maeneo ya urithi wa kitamaduni | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Irina Bokova, ametoa wito kwa pande zote katika mzozo wa Libya kulinda maeneo ya urithi wa kitamaduni wa aina yake katika taifa hilo. Bi Bokova ameutoa wito huo kufuatia ripoti za kutia wasiwasi kwamba vitendo vya uharibifu, ulanguzi na uvamizi dhidi ya urithi wa kitamaduni wa [...]

 Nahodha Kristensen ndiye mshindi wa Tuzo ya Ushupavu ya IMO ya mwaka 2014 | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mwaka mmoja baada ya kunusurika mlipuko uliotishia maisha wa watu 32 kwenye chombo chake, nahodha Andreas Kristensen na wafanyakazi wake wa Seaways Britannia wamepokea tuzo ya Shirika la Kimataifa la Masuala ya Bahari, IMO ya Ushupavu wa Kipekee Baharini ya mwaka wa 2014 katika sherehe iliyofanyika hapo jana. Wakati wa kupokea tuzo na cheti kwa [...]

 WHO yatangaza vifaa vya vipimo rahisi vya kutambua kirusi cha Ebola | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Madaktari wa Umoja wa Mataifa wamesema vifaa ambavyo ni rahisi kuvitumia katika kuchunguza kisa cha mwisho cha ugonjwa wa Ebola vimo mbioni kuundwa. Tangazo hilo ni hatua nyingine katika juhudi za Shirika la Afya Duniani, WHO za kutokomoza ugonjwa huo hatari ambao umetanda huko Afrika Magharibi. Kufikia sasa, jitihada za kuukabili ugonjwa huo nchini Guinea, [...]

 Vituo vya kutibu Ebola Sierra Leone vinazingatia viwango:UNICEF | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Harakati za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola zinaendelea kila uchao wakati huu ambapo idadi ya waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo ikiwa imefikia 5,177 kati ya wagonjwa 14,413 waliothibitishwa. Miongoni mwa nchi zilizokumbwa zaidi ni Sierra Leone ambapo tangu ugonjwa ubishe hodi mwezi Mei mwaka huu zaidi ya watu Elfu Moja wamefariki dunia. Hatua zinachukuliwa [...]

 ISIL imekiuka Shari'ah, imekiuka sheria ya vita na kutenda uhalifu dhidi ya ubinadamu- Kamishna Zeid | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Zeid Ra'ad Al Hussein, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo kwamba, kundi linalotaka kuweka dola la Kiislamu lenye msimamo mkali, ISIL limetenda uhalifu uliokithiri nchini Iraq na kukiuka, siyo tu Shari'ah ya Uislamu, bali pia limekiuka sheria ya kimataifa, ikiwemo sheria ya kivita. Kamishna Zeid amesema [...]

 Ban alaani shambulizi la leo dhidi ya hekalu Jerusalem | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amelaani vikali shambulizi la leo Jumanne Novemba 18 dhidi ya hekalu Jerusalem Magharibi, ambalo limewaua watu wanne na kuwajeruhi wengine kadhaa. Katibu Mkuu ametuma rambi rambi zake kwa familia za wanhanga, na kuwatakia majeruhi nafuu haraka. Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Katibu Mkuu amesema, mbali na [...]

 Mali yaongeza jitihada za kupambana na Ebola | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita, amewataka wananchi kuchukua tahadhari zote katika vita dhidi ya Ebola, akisema kuwa hawatafunga mpaka wa nchi hiyo, lakini akaongeza kwamba hakuna atakaye ruhusiwa kuingia nchini humo pasi na kunawa mikono au kupimwa joto. Taarifa kamili na Abdullahi Boru. (Taarifa Abdullahi) Kama hatua ya kudhibiti kuenea kwa ugojwa huo, serikali [...]

 WHO yatiwa moyo kutosambaa kwa binadamu kwa kirusi kipya cha ndege H5N8 | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema  mlipuko wa hiivi karibuni wa homa ya mafua ya ndege haujaambukiza binadamu na kwamba unaweza kutibiwa kwa dawa zilizopo. Akiongea na waandishi wa habari mjini Geneva daktari wa WHO Elizabeth Mumford amesema kirusi aina ya H5N8 hakitabiriki na kwamba kinafanana na kile kiitwacho H5N1 ambacho kilisababisha magonjwa kwa binadamu [...]

Comments

Login or signup comment.