Idhaa ya Redio ya UM show

Idhaa ya Redio ya UM

Summary: no show description found

Join Now to Subscribe to this Podcast

Podcasts:

 Amani irejee Sudan Kusini ili maisha yaendelee: Kang Kyung-Wha | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu misaada ya kibinadamu Kang Kyung-Wha amesema ni lazima amani irejee Sudani Kusini ili watu warejee nyumbani na kujenga maisha upya. Akizungumza na waaandishi wa habari baada ya ziara yake ya siku tatu nchini humo kiongozi huyo ambaye alitembelaa Sudan Kusini mwaka jana amesema hali ya kibinadamu [...]

 Tanzania inanufaika vilivyo kwa mkutano wa lishe :Dk Rashid | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mkutano kuhusu lishe ukiendelea mjini Roma Italia, wawakilishi mbalimbali wa nchi wameelezea namna unavyonufaisha nchi zao katika mustakabli mzima wa chakula na lishe. Miongoni mwao ni waziri wa afya wa Tanzania Dk Seif Rashid ambaye katika mahojiano maalum na Leda Letra wa radioya Umoja wa Mataifa amesema hii ni fursa kwa nchi yake kujifunza namna [...]

 Mahitaji ya polisi wa Umoja wa Mataifa yameongezeka maradufu: Ladsous | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa, Hervé Ladsous amesema kipindi cha miaka Kumi na Mitano kimeshuhudia kuongezeka kwa kiwango, upeo na umuhimu wa Polisi wa Umoja wa Mataifa. Akihutubia Baraza la Usalama hivi leo, Bw Ladsous amesema ongezeko hilo linatokana na changamoto wanazokumbana nazo wakiwa maeneo ya kazi na hivyo [...]

 UNICEF na washirika wajenga matumaini kwa watoto Kenya | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katika kusaidia kukuza haki na ustawi wa watoto, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau linajenga upya saikolojia za watoto waliofiwa na wazazi wao kutokana na ugonjwa wa Ukimwi nchini Kenya. Mradi huu wa kuwapa matumaini watoto hawa unashuhudiwa kuwa na mafanikio makubwa kwani watoto wanaeleza namna walivyofaniiw akupambana [...]

 Tume ya haki za binadamu yajibu tuhuma nyingi za uvunjwaji wa haki za binadamu Eritrea | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

 Wachunguzi wamenza utafiti nchini Eritrea ambapo baraza la haki za binadamu limelaani kile ilichokiita kuenea kwa mifumo ya uvunjaji wa haki za msingi za binadamu. Tuhuma hizo ni pamoja na mauaji yasiyo halali ,utesaji, ukamatwaji holela,uwekwaji kizuizini na kulazimishwa kujiunga na jeshi. Kwa mujibu wa mkuu wa uchunguzi huo Mike Smith maelfu ya vijana na [...]

 Uwepo wa Papa Francis kwenye ICN2 umenigusa: Makene | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu lishe unaendelea huko huko Roma, Italia ambapo viongozi mbali mbali wanahutubia wakipigia chepuo haki ya chakula na lishe bora. Miongoni mwao ni kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis ambaye uwepo wake kwenye mkutano huo uliibua hisia miongoni mwa washirika wa mkutano na mashuhuda. Mmoja wao ni Boniphace Makene, [...]

 IAEA yasimama kidete kusaidia Afrika dhidi ya Ebola | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA Yukiya Amano amezungumzia hatua ambazo shirika lake limefikia katika kusaidia harakati dhidi ya Ebola kwenye nchi zilizokumbwa na mlipuko barani Afrika. Akitoa ripoti yake wakati wa kikao cha siku mbili cha bodi ya magavana wa shirika hilo kilichoanza Alhamisi huko Vienna, Austria [...]

 Mijadala ni muhimu katika kufikia filosofia ya kweli: UNESCO | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya filosofia Mkuu wa shirika la Umoja wa Matiafa la sayansi, elimu na utamaduni UNESCO Irina Bukova amesema hakuna filosofia ya kweli bila majadiliano. Katika taarifa yake ya kuadhimisha siku hii Bi Bokova amesema  katika dunia ya utandawazi, majadiliano lazima yafungamane na viwango tofauti vya hekima ambazo zimeshawishi watu [...]

 Tija pekee kwenye kilimo haitoshi tuweke na viwanda karibu:Kutesa | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa amesema uwekezaji kwenye sekta ya kilimo uwe zaidi ya kuongeza tija kwenye sekta hiyo ambayo bado muhimu kwa maendeleo ya Afrika na hivyo kuinua kipato na kuweka uhakika wa chakula. Amesema hayo kupitia msaidizi wake Balozi Arthur Kafeero wakati wa tukio lililofanyika kwenye Umoja wa [...]

 Ahadi zilizotolewa kwa GCF ni ishara njema kwa mabadiliko ya tabianchi:Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha ahadi za serikali za kutoa dola Bilioni Tisa nukta Tatu kama mtaji wa mfumo wa miradi endelevu isiyoharibu mazingira, GCF. Ahadi hizo zimetolewa wakati wa mkutano wa ahadi uliofanyika huko Berlin, Ujerumani. Ban amekaririwa na msemaji wake akieleza kuwa ahadi hizo ni kiashiria kuwa serikali zinazidi [...]

 Miaka 25 ya CRC, UNICEF yazindua mradi wa #IMAGINE | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika maadhimisho ya miaka 25 ya mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limezindua mradi wa #IMAGINE unaolenga kuibua matumaini kwa mustakhbali wa watoto. Taarifa kamili na Joshua Mmali… (Taarifa ya Joshua) Nats… Ndivyo tukio hilo lilivyoanza na [...]

 Harakati dhidi ya ugaidi, Kenya yatangaza hatua ilizochukua:Balozi Muli | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Balozi  Koki Muli Grignon amesema uanzishwaji wa miradi yenye lengo la kutokomeza umaskini ni mojawapo ya hatua za serikali za kukabiliana na vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali. Akihutubia Baraza hilo wakati wa mjadala wa ngazi ya juu wa wazi kuhusu ugaidi, wapiganaji mamluki [...]

 Wanawake wabunge Tanzania ni wachapakazi: Anne Makinda | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Wakati kikao cha maandalizi ya mkutano wa maspika wa bunge kikimalizika mjini New York, spika wa bunge kutoka Tanzania Anne Makinda amesema wabunge wanawake nchini humo wamefanya kazi kubwa katika kuleta mabadiliko juu ya mtizamo wa watu kuhusu wanawake kwenye jamii. Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja [...]

 Uzalishaji wa gesi chafuzi ufikiwe katikati au mwisho wa karne:UM | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP imesema ili kuzuia kuongezeka kwa joto kwa nyuzi joto mbili kwa kipimo cha Selsiyasi pamoja na kuzuia athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi ni lazima uzalishaji wa gesi chafuzi ya ukaa duniani upunguzwe ifikapo katikati au mwisho wa karne hii. Kwa mujibu ya ripoti [...]

 Watu ni kigezo muhimu cha maendeleo kwani ndio utajiri halisi wa nchi: Chauwdry | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema wabunge ni muhimu kwa kila sehemu ya ajenda ya kuendeleza amani, maendeleo na haki za binadamu akisema wao ni daraja baina ya wananchi na jamii, taifa na mataifa. Ametoa kauli hiyo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York wakati wa mkutano wa Umoja [...]

Comments

Login or signup comment.