Idhaa ya Redio ya UM show

Idhaa ya Redio ya UM

Summary: no show description found

Join Now to Subscribe to this Podcast

Podcasts:

 Utu na watu viwe msingi wa malengo endelevu:Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amelihutubia Baraza Kuu kuhusu ripoti yake inayotoa mwelekeo wa mchakato wa mjadala wa malengo ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015. Ban amesema katika mchakato wa ripoti hiyo imebainika kuwa licha ya maendeleo kupatikana katika baadhi ya maeneo bado umasikini na ukosefu wa usawa ni [...]

 Bila suluhu la kisiasa Sudan Kusini, hali itazidi kuzorota:OCHA | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mwaka mmoja tangu kuibuka kwa mapigano nchini Sudan Kusini, hali ya kibinadamu inazidi kuzorota na mamilioni ya watu waliokimbia makazi yao bado wamesaka hifadhi kwenye kambi za wakimbizi au misituni wakiwa na hofu ya kurejea makwao. Hiyo ni kauli ya Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kibinadamu, OCHA Kyung-wha [...]

 Tuwezeshe waathirika wa mizozo dhidi ya msongo wa mawazo: Jan Eliasson | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema katika ulimwengu uliojaa majanga na mizozo, ni muhimu kuimarisha uwezo wa watu kukabiliana na hali hizo ili kuweza kumudu mistuko na misongo ya mawazo. Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tatu wa kimataifa wa sera uliondaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya [...]

 Mitandao ya kijamii inawezesha usafirishaji haramu: IOM | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Udhibiti dhidi ya usafirishaji haramu ni mgumu kutokana na wasafirishaji hao kutumia mitandao ya kijamii katika kuratibu shughuli zao na hivyo ni suluhisho la pamoaj linahitajika. Akiongea na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM Leonard Doyle, usafirishaji haramu unakuwa kwa kasi akitolea mfano kuwa mwaka huu pekee [...]

 Barafu kwenye ncha ya kaskazini hatarini kutoweka: WMO | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la  hali ya hewa duniani, WMO limetoa ripoti yake ya mwaka inayosema iwapo kiwango cha joto duniani hakitapungua, barafu katika eneo la ncha ya kaskazini mwa dunia itatoweka. Mkurugenzi Mkuu wa WMO Michel Jarraud amesema onyo hilo linatokana na tafiti zinazoonyesha mwelekeo wa ongezeko la kiwango cha joto duniani ambapo mwaka huu taarifa za [...]

 Kesi dhidi ya Kenyatta, upande wa mashtaka wapewa wiki moja:ICC | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC leo imekataa maombi ya upande wa mashtaka na ule wa utetezi kuhusu hatma ya kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta. Katika maombi yao, upande wa mashtaka ulitaka kesi hiyo iahirishwe huku ule wa utetezi ukitaka kesi hiyo itupiliwe mbali. Badala yake jopo la majaji limetaka upande wa mashtaka uwe umetoa [...]

 WFP yazindua kampeni ya kuchangisha fedha | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Baada ya kukumbwa na ukata na kulazimika kusitisha msaada wa chakula kwa wakimbizi Milioni 1.7 wa Syria, Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limezindua kampen ya saa 72 ya kuchangisha fedha kupitia mitandao ya kijamii. Lengo la kampeni hiyo ni kuchangisha dola Milioni 64 zitakazotumika kununua vocha za msaada wa chakula kwa wakimbizi hao [...]

 UNICEF yakabiliana na Unyanyapaa kwa waathirika wa Ukimwi Kenya | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Unyanyapaa ni tatizo kubwa kwa vijana wanaoambukizwa virusi vya Ukimwi, amesema Grace Muthoni, kiongozi wa taasisi iitwayo Max Facta Youth Group inayojishughulisha na vijana waliopata maambukizi ya ukimwi nchini Kenya. Katika kutatua tatizo la unyanyapaa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linawawezesha vijana hao kwa naman nyingi ikiwamo kujitokeza hadharani kutoa elimu [...]

 Hatua zinaridhisha Liberia juhudi zaidi zahitajika: Nabarro | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mjumbe maalum wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika mapambano dhidi ya Ebola, David Nabarro amekahitimisha ziara yake nchini Liberia, ziara yenye lengo la kutathimini juhudi za kuitokomeza ugonjwa huo, iliyomkutanisha na rais Hellen Johnson Sirleaf na wadau wengine. Baada ya kukamilisha zaira hiyo bwana Nabarro amesema ameridhishwa na kiwango cha makabiliano dhidi ya Ebola [...]

 Shule ya Al Bassir Somalia ni kielelezo cha manufaa ya teknolojia kwa wasioona | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Leo ni siku ya kimataifa ya watu wanaoishi na ulemavu ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema ujumbe wa mwaka huu unaolenga maendeleo endelevu na ahadi ya teknolojia kuimarisha ustawi wa kundi hilo umekuja wakati muafaka. Taarifa kamili na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Ban amesema teknolojia imebadilisha ulimwengu kwa kupanua wigo [...]

 Maendeleo ya teknolojia yajumuishe watu wenye ulemavu:Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Leo ni siku ya kimataifa ya watu wanaoishi na ulemavu ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ujumbe wa mwaka huu unaolenga maendeleo endelevu na ahadi ya teknolojia kuimarisha ustawi wa kundi hilo umekuja wakati muafaka. Ban amesema teknolojia imebadilisha ulimwengu kwa kupanua wigo wa fursa lakini bado idadi kubwa ya watu [...]

 Harakati dhidi ya Ebola, Afrika yaipatia FAO msaada wa fedha | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limepokea dola Milioni Moja na Nusu kutoka mfuko wa mshikamano wa bara la Afrika kwa ajili ya kuimarisha shughuli za kilimo na uhakika wa chakula huko  Guinea, Liberia na Sierra Leone ambako Ebola imeleta madhara zaidi.Kwa mujibu wa FAO kila nchi itapatiwa dola Laki Tano wakati  huu ambapo [...]

 Chanjo ya Pepopunda yawezesha ustawi wa watoto Kenya | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya wanatoa huduma ya chanjo kwa ugonjwa usio wa kuambukiza wa pepopunda ikiwa ni sehemu ya mikakati ya shirika hilo katika kuimarisha afya na ustawi wa watoto ulimwenguni. Ungana na Amina Hassan katika makala inayokusimulia kwa kina namna [...]

 WFP kupeleka msaada zaidi wa chakula Sudan Kusini: UM | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP linatarajia kupeleka zaidi ya tani 400 ikiwa ni ziada ya chakula cha msaada wa chakula kwa kutumia basi Sudani Kusini. Akiongea na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephanie Dujarric amesema msaada huo utatoka jimbo la White [...]

 Mpango wa makazi kusaidia wahanga wa vita huko Bosnia-Herzegovina:UNHCR | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na wadau wake wa kimataifa ikiwemo muungano wa Ulaya umeandaa mpango wa makazi kwa ajili ya makumi ya maelfu ya wananchi waliopoteza makazi yao wakati wa miongo miwili ya vita huko Bosnia-Herzegovina. Mwakilishi mkazi wa UNHCR huko Bosnia- Herzegovina, Andrew Mayne, amesema mpango huo [...]

Comments

Login or signup comment.