Idhaa ya Redio ya UM show

Idhaa ya Redio ya UM

Summary: no show description found

Join Now to Subscribe to this Podcast

Podcasts:

 Onyesho la mitindo ya mavazi ya Palestina lavutia | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mitindo ya mavazi hutoa taswira halisi ya utamaduni wa jamii husika. Kama huifahamu jamii fulani waweza kuitambua kwa kuangalia mitindo ya mavazi kwani husema kila kitu. Taifa la Palestina hivi karibuni limedhihirisha hilo kupitia onyesho kabambe katika Umoja wa Mataiafa lililowaleta pamoja watu mbalimbali hususani kutoka nchini humo. Ungana na Abdullahi Boru katika makala itakayokupa [...]

 Tupunguze kiwango cha mlo kadri jua lizamavyo: Mtaalamu akizungumzia Kisukari | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Tarehe 14 mwezi Novemba kila mwaka ni siku ya kisukari duniani. Siku hii ni Ikiwamahsusi kutathmini mwelekeo wa matibabu dhidi ya ugonjwa huo wenye aina mbili; Kisukari aina ya kwanza ambayo ni ya kurithi na aina ya pili inayotokana na mwili kushindwa kutumia vizuri kichocheo cha Insulin. Ujumbe wa mwaka huu ni maisha yenye afya [...]

 Kirusi cha polio chazuka Sudan Kusini na Madagascar | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

  Shirika la Afya Duniani, WHO, limetangaza leo kuthibitishwa kuzuka kwa matukio mawili tofauti ya kirusi cha polio kitokanacho na kutopata dozi tosha ya chanjo ya mdomoni (OPV) katika nchi za Sudan Kusini na Madagascar. Nchini Sudan Kusini, visa viwili vya ugonjwa huo aina ya cVDPV2 vimethibitishwa katika jimbo la Unity, ambako waathiriwa wawili walianza [...]

 Sierra Leone yapata vituo vipya 10 vya kutibu Ebola | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, mwishoni mwa wiki hii linazindua vituo vipya 10 vya kijamii vya kutoa tiba dhidi ya Ebola chini Sierra Leone. Kila kituo kitakuwa na vitanda vinane ambapo UNICEF ambayo ndiyo imevijenga imesema vitaongeza idadi ya vitanda vinavyohitajika ili kuboresha huduma dhidi ya Ebola kwenye wilaya ya Bombali, [...]

 Uwajibishwaji haukwepeki DPRK: Mtaalamu | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

  Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya watu wa Korea (DPRK) Marzuki Darusman amesema suala la uwajibishwaji kwa wanaotenda uhalifu kinyume na binadmau nchini humo linasalia ajenda muhimu Akiongea baada ya kuhitimisha ziara yake mjini Seoul, Bwana Darusman amesema maoni hayo yanakuja muda mfupi kabla ya [...]

 Ukatili wa ISIS kwa wananchi ni wa kupindukia: Tume | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Raia wa Syria wanaoishi kwenye maeneo yanayodhibitiwa na kikundi cha kigaidi kinachotaka kuunda dola ya kiislamu huko Syria,  ISIS wanakabiliwa na vitendo vya ukatili na kulazimishwa kushiriki mafunzo ya kikundi hicho. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti inayotokana na uchunguzi uliofanywa na Tume huru ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza madhila yanayokumba raia huko Syria, [...]

 Vijana kushirikishwa katika kuleta mabadiliko siku ya idadi ya watu:UNFPA Tanzania | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Kuelekea siku ya kimataifa ya idadi ya watu November 18 imeelezwa kuwa vijana wakiwezeshwa na kujumuishwa  katika uzalishaji wanaweza kuchangia katika pato la nchi. Katika mahojiano na afisa mawasiliano wa mfuko wa idadi ya watu nchini  Tanzania UNFPA , Sawiche Wamunza,  afisa wa idadi ya watu na maendeleo Samweli Msokwa amesema UNFPA itaadhimisha siku hiyo [...]

 Kipindi cha mpito cha kiraia Burkina Faso kianze haraka iwezekanavyo: Ibn Chambas | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Afrika Magharibi, Dkt. Mohammed Ibn Chambas amesema mazungumzo ya kurejesha utulivu nchini Burkina Faso yanaendelea vyema kati ya vyama vya siasa, vikundi vya kiraia na wananchi upande mmoja na viongozi wa kijeshi. Akihojiwa na Derrick Mbatha wa Radio ya Umoja wa Mataifa, Dkt. Chambas amesema hadi [...]

 Vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake nchini Afghanistan vimeenea:Manjoo | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na  ukatili dhidi ya wanawake Rashida Manjoo amesema kwamba ukatili dhidi ya wanawake ni changamoto na  kitu kilichoenea nchini Afghanistan. Bi. Manjoo ambaye amemaliza ziara ya wiki moja nchini humo akichunugiza hali ilivyo ametolea wito serikali ya Afghanistan na jamii ya kimatifa kuhakikisha kwamba washiriki wa [...]

 Vifo vya surua vyapungua kidogo, WHO yaonya mkwamo wa kutoa chanjo | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

  Vifo vitokanavyo na surua vimepungua kidogo kwa asilimia 20 mwaka jana na hivyo angalizo limetolewa kuwa kuna hatari ya ugonjwa huo kuibuka upya limesema shirika la afya ulimwenguni WHO. Kwa mujibu wa takwimu za WHO zaidi ya watu 145,000 walifariki dunia  kutokana na ugonjwa huo mwaka 2013 na idadi hiyo imepungua hadi 122,000 mwaka [...]

 Wakimbizi Iraq wahangaika kujiandaa kwa majira ya baridi kali | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Juhudi zinaendelea sasa nchini Syria, Iraq na nchi jirani, kuwaandaa wakimbizi wa kigeni na wa ndani kwa msimu wa baridi. Lakini watu milioni moja waliolazimika kuhama makwao Syria na Iraq, na kwingineko katika ukanda hawataweza kupata usaidizi kwa sababu ya upungufu wa dola milioni 58.4 za ufadhili kwa ajili ya mipango ya majira ya baridi. [...]

 Wanafunzi katika shule za UNRWA wafanya vyema na kuvuka kiwango: Ripoti | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ripoti mpya ya bank ya dunia inaonyesha kuwa wanafunzi wanaohudhuria masomo katika shule za shirika la Umoja wa Mataifa linalotoa usaidizi kwa wakimbizi wa Palestina UNRWA wanafanya vyema wakivuka kiwango cha kimataifa cha tathimini za kimataifa cha Hesacu na masomo ya sayansi (TMSS). Ripoti ya benki ya dunia iliyopewa jina kujifunza katika hali tete inaeleza [...]

 Ban akiwa Myanmar akutana na Aung San Suu Kyi | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliyeko ziara huko Mashariki ya mbali amekuwa na mazungumzo na mwanaharakati na Mwenyekiti wa chama cha National League for Democracy, NLD nchini Myanmar Angu San Suu Kyi. Wakati wa mazungumzo kati yao, Ban amepongeza dhima ya Suu Kyi kama kiognozi wa upinzani na mchango wake wa dhati [...]

 Makundi nchini Mali yasema yamechoshwa na machafuko: MINUSMA | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Kaimu Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA  ambaye anaelekea nchini Algeria kwa ajili ya mazungumzo ya kusaka amani nchini Mali  Arnaud Antoine Akodjenou amesema jamii nchini humo imechoka na machafuko yanayokwamisha huduma za kijamii. Akihojiwa na kaimu mkuu wa mawasiliano wa MINUSMA Olivier Salgado, kiongozi huyo ambaye amekutana na makundi mbalimbali [...]

 Uhifadhi wa bahari na bayonuai uko katika mkondo sahihi:Ripoti | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP imesema dunia iko katika mkondo sahihi katika kufikia malengo ya mwaka 2020 ya kuongeza maeneo ya hifadhi ardhini na baharini ili kuhakikisha kwamba maeneo muhimu kwa ajili ya bayoanuai na huduma za mazingira yanapewa kipaumbele kwa ajili ya ulinzi chini ya usimamizi wa mazingira sawia. [...]

Comments

Login or signup comment.